Chid Benz afungukia muonekano wake wa nywele

0
68

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Chid Benz amefunguka na kusema kuwa ameamua kubadilisha muonekano wake wa nywele kwasababu ni wakati wake wa kubadilika lakini akuiga mtu yoyote.

Chid ametoa kauli wakati alipohudhuria kwenye sherehe ya kuzaliwa Diamond iliyofanyika Tandale ambapo alitoa zawadi na kuwasaidia watoto waishio mazingira magumu maeneo ya Tandale.

Chid amesema kuwa amepaka nywele zake rangi kwa maamuzi yake mwenyewe na sio kama anawaigiza wasani wanaotoka Jamuhuri ya Demokrasia ya Congo.

Pia amesema kuwa watu wanafikra tofauti na kupenda kuongea mambo mengi, mtu anapofanya kitu wanahisi tu atakuwa amewaiga watu wengine lakini kwa upande wake hakuna kitu kama hiko.

Vile vile Chid alimuongelea Diamond kutokana na mchango wake kwa jamii ambapo amesema amefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuufikisha Muziki wa Bongo Fleva mbali sana.

LEAVE A REPLY