Chid Benz afunguka kuhusu mitandao ya kijamii

0
108

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Chid Benz amefunguka na kusema watu wake hawamruhusu yeye kutumia mitandao ya kijamii kwa sababu, aliambiwa hatakiwi kuyaona yale yanayoendelea duniani.

Sababu ya kuambiwa hivyo ni kukazania zaidi kwenye masuala yake ya kazi kuliko yale yanayoendelea duniani kupitia mitandao ya kijamii.

“Ukitaka kusema kuhusu mimi hakikisha wewe umekamilika zaidi yangu, pia siwezi kubishana na mtu wa mitandaoni kama amenitukana.

Japo kuna muda huwa naangalia kwenye mitandao lakini watu wangu hawaniruhusu kufanya hivyo maana niliambiwa sitakiwi kuiangalia hii dunia na mambo yanayoendelea ninachotakiwa kufanya ni kazi tu” ameeleza Chidi Benz.

Pia Chidi Benz ameendela kusema kwa sasa hata simu zake hashiki yeye kuna mtu anaitwa Saidi ndiyo anazimiliki na hayupo kwenye mambo ya mitandao.

LEAVE A REPLY