Chemical aogopa kuumizwa na mapenzi

0
322

Mkali wa hip hop Bongo kwa upande wa wanawake, Chemical amefunguka na kusema kuwa haweki nguvu nyingi kwenye mapenzi kwa sababu anaogopa kuumizwa na wanaume.

Chemical amesema kuwa kama msichana ana hisia za mapenzi na anajua kupenda, ila anahofia kuumizwa hivyo hawezi nguvu nyingi kwenye masuala ya mapenzi.

Mwanamuziki amesema kuwa yeye kama msichana na kama binadamu ana hisia za mapenzi ila wanaume wa siku hizi ni waongo na wanaweza kukuumiza muda wowote hivyo siyatilii mkazo masuala ya mapenzi.

Chemical amefunguka hayo baada ya tetesi kuwa mpenzi wake alikuwa akiishi naye pamoja ambaye pia anayemsimamia, kutokea kutoelewana kiasi cha kususa kumsimamia kazi zake bila taarifa yoyote, licha ya kwamba alisaini naye mkataba.

Mwanamuziki huyo kwasasa anatamba na ngoma mpya inayokwenda jina la ‘Achana na Mimi’ ambayo ameshirikiana na mwanamuziki mwenzake wa hip hop, Pink.

LEAVE A REPLY