Chemical akiri muziki wa Singeli kumpungizia mashabiki

0
478

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Chemical amefunguka na kusema kuwa heshima ya muziki wake ilishuka kwa mashabiki wake baada ya kuanza kuimba nyimbo za Singeli.

Chemical alisema suala la kuimba Singeli lilitoka kwa menejimenti yake aliyoachana nayo lakini kwa upande wake anaamini muziki wao unaweza kuwa umemuongezea mashabiki kidogo kwenye upande huo.

Pia amesema kuwa  lakini mashabiki wake ambao tayari walikuwa wamekwisha mpokea vizuri kwenye Hip Hop, wamemshusha thamani.

Amesema kuwa ukweli ni kwamba aamini sana kupitia Muziki wa Singeli, ninaamini kwamba muziki wangu niliokuwa ninaufanya ulikuwa ni mkubwa kuliko Singeli.

Chemical aliachia wimbo uitwao Kama Ipo Ipo Tu aliyoshirikiana na Msaga Sumu ambao kimsingi mwenyewe ameulalamikia kuwa umemshushia heshima.

LEAVE A REPLY