Chelsea yakamilisha usajili wa Ross Barkley kutoka Everton

0
338

Chelsea imekamilisha usajili wa kiungo wa kimataifa wa Uingereza kutoka klabu ya Everton, Ross Barkley.

Uo unakuwa usajili wa kwanza kufanywa na Chelsea katika dirisha hili dogo la usajili kwa ajili ya kuimalisha kikosi chao.

Barkley amekuwa mchezaji ambaye amekuwa akiwindwa na klabu hiyo ya Chelsea kwa muda na hatimaye katua Stamford Bridge na atavaa jezi ya namba nane 8.

Kiungo huyo amenunuliwa kwa dau la pauni milioni 15 na ataitumikia klabu hiyo kwa muda wa miaka mitano na nusu.

Barkley hajaonekana uwanjani kwa muda wa miezi saba tangu apate majeraha agosti 2017.

Meneja wa klabu hiyo ya Chelsea amesema kuwa mchezaji huyo ni mdogo na bado ana muda mwingi wa kuwa mchezaji bora.

LEAVE A REPLY