Chege akanusha kuwa na bifu na Temba

0
694
Chege akiwa na Temba

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Chege Chigunda amesema kuwa hana mgogoro na msanii mwenzake Temba licha ya wawili kutofanya wimbo wa pamoja kwa muda mrefu.

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Chege Chigunda amenyoosha maelezo kuhusu kile kinachoendelea kwa sasa kwenye mitando ya kijamii, kuhusu yeye na msanii mwenzake wa siku nyingi, Mh.Temba.

Chege amesema kuwa ni mipango tu ya kazi, kuna kufanya ngoma pamoja na kufanya ‘collabo’, hicho ndio kinachofanya watu waone wana tofauti lakini hatuna tofauti yotote zaidi ya kubadilisha mfumo wa kazi,

 Pia msanii huyo amesema kuwa “hizo ni stori za watu, mimi ninavyoelewa siyo hivyo watu wanavyofikiria na wanavyoongea. Huwezi kumzuia mtu kuongea”.

Taarifa za wasanii hao kutokuwa pamoja zimekuja mara baada ya Chege kufuta picha zote alizowahi kupiga na Mh.Temba kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram, na kutoonekana wakiwa pamoja kwa muda mrefu hivi sasa.

Chege na Temba ni wasanii na marafiki wa muda mrefu ambapo walikuwa katika kundi la TMK Wanaume Family lililokuwa na maskani yake Temeke, Dar es Salaam.

LEAVE A REPLY