Cheed akanusha kujiunga Konde Gang

0
88

Aliyekuwa mwanamuziki wa Kings Music Records, Cheed amekanusha kujiunga na lebo ya Harmonize, Konde Gang licha ya kutoka Kings Music.

Kauli ya mwanamuziki huyo imekuja baada ya kuhusishwa kujiunga na lebo ya Harmonize baada ya kuachana na Alikiba.

Cheed amesema suala hilo halina ukweli wowote na hata yeye analisikia mitandaoni japo kwa sasa hivi anashambuliwa kwa matusi baada ya kutoka kwa Alikiba.

Pia amesema kuwa “Hakuna mtu ambaye ametushika akili tutoke Kings Music ni stori ambazo zinatengenezwa kutokana na hili tukio, suala la sisi kwenda Konde Gang halina ukweli wowote japo hata mimi nalisikia kwenye mitandao.

Pia ameongeza kwa kusema kuwa lakini kwa sasa hakuna ukweli juu ya hilo, na sasa hivi nashambuliwa kwa kutukanwa sana hadi nazima simu ila mimi nachukulia kama changamoto”.

LEAVE A REPLY