Charlize Theron : Uzembe na ubaguzi ndio unasababisha UKIMWI

0
148
Actress Charlize Theron gives her speech at the at the AIDS 2016 - Opening Session on July 18, 2016 in Durban
Staa wa filamu aliyeshinda tuzo ya Oscar, Charlize Theron aliyezaliwa na kukulia nchini Afrika Kusini ameilaumu jamii ya nchi hiyo kwa kuendelea kuwepo kwa ugonjwa wa UKIMWI.
Staa huyo mwenye miaka 40, alikuwa akiwahutubia madaktari takribani 18,000, watafiti, wanaharakati, watunga sera na wakuu wan chi kwenye ufunguzi wa kongamano la 21 la kimataifa la UKIMWI kwenye jiji la Durban nchini Afrika Kusini.
Theron ambaye ni balozi wa Umoja wa Mataifa wa Amani na mwanzilishi wa mradi wa ‘Charlize Africa Outreach’ unaowalenga vijana wa Afrika Kusini wenye maambukizi ya virusi vya Ukimwi alisema:
‘Tunathamini maisha yetu kuliko tunavyothamini maisha ya wengine’.
Theron alionyesha kusikitishwa kwake na idadi kubwa ya watu wenye maambukizi ya VVU wanaofikia milioni 2.1 na bado maambulizi mapya yanaendelea kutokea kila siku licha ya kuwa na nyenzo zote za kuzuia kuenea kwa maradhi haya.
‘Tunawathamini wanaume kuliko wanawake……..weupe kuliko weusi…..na wakubwa kuliko watoto’.

LEAVE A REPLY