Charles Baba afunguka kuhusu ndoa yake

0
80

Muimbaji wa bendi ya Twanga Pepeta, Charles Baba amefanya amefunga ndoa na mpenzi wake ambaye anafahamika kwa jina la Mariam baada ya kudumu naye kwa takribani miaka kumi katika uchumba wao.

Sherehe ya ndoa hiyo imefanyika siku ya Jumamosi jijini Dar es Salaam ambapo iliudhuriwa na watu maarufu kibao akiwemo mwanamuziki nyota wa Bongo Fleva, Ali Kiba.

Baada ya sherehe Charles amesema kuwa hayuko tayari kuongea suala lolote kuhusu ndoa zake zilizopita kwa sasa kipaumbele chake ni mke wake Mariam na kusema kwamba anampenda sana na hawezi kumuacha kamwe.

Mke wa Charlse nae amesema kuwa anaampenda sana mume wake kwani ni chaguo lake na amempenda mwenyewe awezi kubadilisha mawazo yake na anapenda watu wafahamu kwamba amekuwa katika mapenzi na mume wake tangu mwaka 2005 mpaka sasa walipoamua kufunga ndoa.

Charles Baba amemalizia kwa kusema kwamba pamoja na kwamba imezoeleka kwa wasanii wakioa wanapotea katika muziki lakini kwa upande wake hawezi kuacha muziki kwa kuwa ndio kazi yake lakini pia mke wake amekuwa akimsapoti kwa kiasi kikubwa katika kazi yake hiyo.

LEAVE A REPLY