Chameleone akanusha taarifa za mkewe kudai talaka mahakamani

0
280

Mwanamuziki nyota wa Uganda, Jose Chameleone amekanusha tetesi kwamba mkewe Daniella Atim amekwenda mahakamani kudai talaka.

Taarifa zilizosambaa mitandaoni kwamba Daniella alidai kwa kutokuwa na furaha na ndoa yake kutokana na manyanyaso na vipigo anayoyapata kutoka kwa muimbaji huyo.

Chameleone ameamua kuvunja ukimya kupitia mtandao wa Facebook kwa kurusha video ya dakika 53 akiongelea mengi kuhusu familia yake, ambayo inaonekana kuwa na furaha tofauti na yanayozungumzwa.

Kupitia video hiyo Chameleone amesema “Kuna habari nyingi zimesambaa zinazohusu mimi na familia yangu.

Amesema kuwa ‘Siwezi kusema kubwa lolote lakini nachotaka kusema ni kuwa sina talaka wa hakuna anayedai talaka,.

Kumbuka mimi ni mkatoliki, mkatoliki akifunga ndoa hawezi kuachana mpaka kifo kitakapowatenganisha.

LEAVE A REPLY