Chadema wavamia ofisi za tume ya taifa ya uchaguzi

0
155

Mwenyekiti CHADEMA Freeman Mbowe na viongozi wengine wa chama wamekwenda ofisi ya NEC kushinikiza wapewe viapo na vitambulisho vya mawakala wao, huku wakidai mawakala wa CCM wameshapewa.

Msafara huo wa viongozi ulipofika ofisi hizo kwa lengo la kukutana na Mkurugenzi wa Tume hiyo, Ramadhan Kailima waligonga mwamba baada ya watumishi wa NEC kudai kuwa Mkurugenzi huyo hayupo ofisini.

Viongozi hao waligoma kuondoka katika ofisi hiyo mpaka baadae Mbowe alipoongea na Mkurugenzi huyo kwa simu na kukubaliana mambo kadhaa.

Mbowe alisema amefika ofisini hapo kutokana na kuwa na mawasiliano madogo na NEC. Kailima ameahidi kuzungumza na wenzake katika Tume kuona watafanya nini na kuwajibu CHADEMA leo jioni kwa njia ya simu na maandishi.

Miongoni mwa viongozi waliokuwepo ni Halima Mdee, Esther Bulaya, John Heche, Peter Msigwa, John Mnyika na mgombea wa Jimbo la Kinondoni, Salim Mwalim

LEAVE A REPLY