Chadema wadai hawana imani na upelelezi wa Polisi dhidi ya tukio la kushambuliwa kwa Tundu Lissu

0
119

Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara na Wakili wa kujitegemea Tanzania. Prof Abadallah Safari amesema wao kama CHADEMA hawana imani na uchunguzi utakaofanywa na jeshi la polisi au serikali kuhusu shambulio la kujaribu kumuua Mbunge Tundu Lissu.

Akizungumza na wanahabari wakati wakitoa taarifa ya kamati kuu kupitia kikao walichokaa mwishoni mwa wiki iliyopita, Prof. Safari amesema kuwa wao hawana nia mbaya ya kutaka uchunguzi kufanywa na wachunguzi wa mambo ya nje lakini hii ni kutokana jinsi tukio lilivyotokea.

Pamoja na hayo Prof. Safari amedai anamshangaa sana Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini , IGP Simon Sirro, kwa kauli yake ya kwamba Tundu Lissu hakufika kuripoti tukio la kufuatiliwa na watu asiowajua na kusema kuwa huko ni kutojua sheria ya mmwenendo wa makosa ya jinai.

Amesema kuwa Sheria hiyo inaeleeza namna jeshi lapolisi linavyotakiwa kufanya kazi zake na kwamba kutokana na aslimia 90 ya wananchi basi jeshi la polisi kazi yake ni kufuatilia  na kufanya upelelezi juu ya taarifa kwani wao ni walinzi wa amani na kuongeza kwamba Lissu tayari alieleza kila kitu lakini polisi hawakujali.

Mbali na hayo Katibu Mkuu wa Chama hicho Dkt. Vicent Mashinji ameeleza kwamba kwa sasa wanachohakikisha ni kwamba hospitali aliyopo Lissu inazidi kuimarishwa ulinzi lakini pia hatoweza kuzungumzia hali yake kwa undani kutokana pia na kuwepo watu wasiokuwa na nia njema.

LEAVE A REPLY