Card B aweka rekodi Billboard

0
222

Mwanamuziki nyota wa Marekani, Cardi B amekamata rekodi nyingine tena kwenye chati za Billboard Hot 100 ambapo wimbo wake wa ‘I Like It’ aliowashirikisha Bad Bunny na J Balvin umeweza kukaa kwenye chati hizo kwa miezi kumi .

 Cardi B anashikilia rekodi hiyo kutokana na wimbo huo kuwa wa msanii wa kike uliokaa kwa wiki nyingi zaidi katika historia ya chati hizo na kutajwa kuwania kipengele kimoja cha ‘Record Of The Year” kwenye tuzo za Grammy 2019.

Ngoma hiyo inapatikana kwenye album ya Cardi B inayojulikana kwa jina la Invasion of Privacy ikiwa wimbo huo ulitoka May 29, 2018.

Wimbo wake wa pili kupata nafasi katika chart za Billboard Hot 100 wakati wimbo wa Bodak Yellow uliwahi kushika namba moja mwezi October 2017.

LEAVE A REPLY