Card B aonyesha pete ya ndoa aliyovalishwa na Offset

0
101

Rapa wa kike anayetikisa kwenye muziki wa Hip Hop kutoka Marekani, Cardi B ameonesha pete yake ya uchumba aliyovalishwa na rapa mwenzake, Offset.

Wawili hao ambao wote wana miaka 26, wamefanikiwa kupata mtoto mmoja, lakini mwishoni mwa mwaka jana walizinguana kila mmoja akawa na maisha yake.

Katika Tamasha la BelAir lililofanyika katika Sikukuu ya Valentine’s Day walionekana kurudiana huku Cardi B akianika pete yake ya uchumba.

Wawili hao kwasasa wameamua kuonyesha mapenzi yao wazi wazi baada ya kumaliza mgogoro wao ambao uliwatenganisha.

Wapenzi hao wamejaliwa kupata mtoto mmoja ambaye amezaliwa mwishoni mwa mwaka jana.

LEAVE A REPLY