Canavaro afiwa na mtoto wake wa miezi miwili

0
229

Beki wa mabingwa wa ligi kuu Tanzania Bara, Nadir Haroub ‘Canavaro’ amepatwa pigo baada ya kufiwa na mwanawe wa miezi miwili.

Msiba umetokea wakati beki huyo akiitumikia klabu yake iliyoko nchini Shelisheli kucheza mechi za kimataifa dhidi ya St Louis.

Anuary Nadir aliyekuwa na umri wa miezi miwili amefariki usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam.

Cannavaro anatarajia kuwasili nchini leo akitokea Shelisheli ambako amekwenda kuitumikia Yanga katika mechi ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya St Louis.

LEAVE A REPLY