Caf na Total zaingia mkataba wa miaka 8

0
93

Shirikisho la soka la Afrika (Caf) limeingia mkataba wa udhamini kwa miaka nane zaidi na kampuni kubwa ya gesi na mafuta ya Total ya Ufaransa.

Udhamini huo unahusisha mashindano ya timu za taifa na mashindano ya ya kimataifa ngazi za vilabu.

Mkataba huo mpya unatarajia kuanza rasmi kwenye mashindano yajayo ya mataifa ya Afrika yanayotarajiwa kufanyika mwakani nchini Gabon.

Bado thamani halisi ya mkataba huo haijawekwa wazi na taasisi zote mbili.

Kampuni ya Total imechukua nafasi hiyo ya udhamini baada ya mdhamini wa awali, kampuni ya mawasiliano ya Orange unaomalizika mkataba wake mwishoni mwa mwaka huu.

LEAVE A REPLY