Bwana Misosi afunguka alivyomsaidia Harmonize

0
38

Mwanamuziki mkongwe wa Bongo Fleva, Bwana Misosi amesema amewasaidia baadhi ya wasanii kama Man X na Harmonize kwenye kazi zao bila hata ya kuwadai pesa.

Misosi amesema beat la wimbo wake wa nitoke vipi limetumiwa na Man X, pia beat lake la mabinti wa kitanga ametumia Harmonize kwenye wimbo wake wa ‘never give up’.

Amesema kuwa “Kuna wasanii wametumia mgongo wangu kwenye kazi zao kama Man X ametumia beat la wimbo wangu wa nitoke vipi.

 Pia wimbo wa ‘Never Give Up’ ya Harmonize ni beat langu kwenye wimbo wa mabinti wa kitanga, Harmonize alitaka kunilipa nikamwambia gharama zake hataziweza”.

Bwana Misosi amesema nyimbo zake za nitoke vipi na mabinti wa kitanga zilimpa mafanikio makubwa na kumfanya kufahamika ndani na nje ya Tanzania.

LEAVE A REPLY