Bushoke akanusha kuwa na bifu na Q-Chilla

0
232

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Bushoke amefunguka na kukana taarifa zakugombana na mwanamuziki mwenzake, Q-chief na kudai wanaweza kutofautiana lakini siyo kuzinguana kabisa.

Bushoke amesema hayo baada ya kuwepo fununu kuwa wakongwe hao kwa sasa ni kama paka na panya licha ya kuwa karibu hapo awali na hata kurekodi wimbo mmoja studioni lakini mpaka sasa kazi hizo zimefungiwa studio.

Bushoke amesema kuwa “Some times’ tunaweza kutofautiana lakini siyo kivile kwa hiyo namshukuru Mwenyezi Mungu yaani tupo karibu hata huko kutofautiana inawezekana mmoja wetu siku ameamka vibaya kwa hiyo ndio vitu hivyo lakini kugombana hatujawahi.

Baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu kumekuwa na tetesi kwamba wasanii hao wakongwe Bushoke na Q- chillah hawapatani hata kidogo licha ya kuwa marafiki hapo awali.

Wawili hao wamefanya project ambazo walikuwa wanafanya Bushoke na Q-chillah zinashindwa kutoka hadi leo jambo lililopelekea Bushoke kuendelea mbele na kutoa nyimbo yake mwenyewe inayoitwa ‘Ngoma ya ukae’.

LEAVE A REPLY