Bushoke afunguka sababu ya kuhamia Dodoma

0
36

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Bushoke amesema hajalikimbia Jiji la Dar Es Salaam kwa sababu ya ushindani bali kuna kelele nyingi na yeye hapendi kelele hivyo anahitaji muda wa kupumzika na hapendi kuongeaongea.

msanii huyo ambaye kwa sasa anaishi Jijini Dodoma baada ya kuamua kuishi huko licha kuwa na umaarufu mkubwa kwenye muziki.

“Hakuna ushindani wowote kuna kelele nyingi halafu wengine hatupendi kelele tunahitaji muda wa kupumzika, kwa anayesema nimekimbia Dar Es Salaam atakuwa hajui kuchambua mambo vizuri na mimi sipendi sana kuongeaongea” amesema

Bushoke”Dodoma sasa hivi limeshakuwa Jiji sio kama kijiji kwamba useme amekimbilia Dodoma, huku kila msanii anakuja kwa hiyo kwa msanii yeyote ambaye anahisi nimekimbia atakuja huku halafu ataona kama kweli nimekimbia au nimekuja kupunga upepo” ameongeza

LEAVE A REPLY