Bunge la Tunisia lamuondoa madarakani Waziri Mkuu – Habib Essid

0
117

Bunge la Tunisia limepiga kura ya kukosa imani na waziri Habib Essid na kuomba mtaalamu huyo wa uchumi aondolewe kwenye wadhifa wake.

Jumla ya wabunge 188 bila kujali vyama vya siasa wanavyotokea walimpigia kura ya kutaka ang’olewe huku wabunge watatu tu wakipiga kura ya kuwa na imani nae.

Nchi ya Tunisia inakabiliwa na hali ya mdororo wa uchumi na mwezi uliopita rais wan ci hiyo, Beji Caid Essebsi aliunda serikali ya pamoja kwa lengo la kukabiliana na mdororo huo.
Bw. Essid amekuwa madarakani kwa kipindi cha chini ya miaka miwili amekuwa wakikabiliwa na malalmiko na ukosoaji mkubwa kutoka kwa wapinzani wake kwa kinachodaiwa kuwa ni kushindwa kufanikisha mabadiliko ya uchumi.

Hali ya ajira kwenye taifa hilo imekuwa mbaya zaidi huku zaidi ya robo tatu ya vijana wakiwa hawana ajira.

Hali hiyo ya uchumi imekuwa mbaya tangu kutokea kwa mapinduzi ya mwaka 2011 wakati rais Zine al-Abidine Ben Ali alipong’olewa madarakani.

LEAVE A REPLY