Bujumbura: Mwanahabari wa Burundi ashinda tuzo

0
166

Mwandishi wa habari wa Burundi, Eloge Willy Kaneza amefanikiwa kushinda tuzo ya kimataifa ya uandishi wa habari wa kijasiri.

Kaneza na wenzake wameshinda tuzo hiyo kwa kufanikiwa kupata mbinu ya kiubunifu ya kupambana na ukandamizaji kwa kutumia teknolojia za mitandaoni kuripoti habari.

Kwa mujibu wa taarifa ya waandaaji wa tuzo hiyo ya Peter Mackler Award for Courageous and Ethical Journalism walisema mbinu ambayo imetumiwa na Kaneza imesaidia kwenye mapambano dhidi ya ukandamizaji nchini humo.

Bw. Kaneza  amekuwa taswira ya chombo cha SOS Media Burundi, kinachowajumuisha waandishi wa habari wasiotaka kufahamika ambacho kiliundwa kufuatia kufungwa kwa vituo vya redio mwaka 2015 baada ya jaribio lililoshindwa la kumpindua rais Pierre Nkurunzinza.

Waandaaji wa tuzo hizo wamedai kuwa mshindi huyo, Kaneza na wenzake wamekuwa wakifanya kazi zao katika mazingira magumu sana wakitumia simu za mikononi na applications zilizomo kwenye simu hizo kwaajili ya kufanikisha kazi zao.

Wamekuwa wanahabari tegemezi kwa raia wa Burundi waishio ndani na nje ya nchi hiyo.

LEAVE A REPLY