Bruno Mars ang’ara tuzo za Gramy, achukua sita

0
167

Bruno Mars ameng’ara kwenye utaoji wa tuzo za Gramy baada ya kunyakua tuzo sita usiku wa kuamkia leo.

Moja ya tuzo alizoshinda mwanamuziki huyo ni albam bora ya mwaka kupitia albam yake ya ’24k Magic’ baada ya kuwashinda wasanii kama vile Jay Z na Kendrick Lamar.

Kendrick Lamar akipokea tuzo yake
Kendrick Lamar akipokea tuzo yake

Msanii mwengine aliyechukua tuzo nyingi ni Kendrick Lamar ambapo ameshinda tuzo tano moja wapo ikiwa ni tuzo bora ya Rap nchini humo.

Sherehe za utoaji wa tuzo hizo umefanyika katika ukumbi wa Madison Square Garden jijini  New York City.

LEAVE A REPLY