Brexit: Opel kupunguza saa za kufanya kazi Ujerumani

0
98

Kampuni ya kutengeneza magari ya nchini Ujerumani, Opel plans imepanga kupunguza muda wa wafanyakazi wake kufanya kazi kwa mwaka huu kwasababu inatarajia anguko la mauzo kutokana na Uingereza kujitoa kwenye Umoja wa Ulaya.

Msemaji wa kampuni hiyo amedai kuwa takribani wafanyakazi 5,000 kwenye karakana za Ruesselsheim na Eisenach wataathiriwa na hatua hiyo.

Opel ni kampuni inayomilikiwa na kampuni kubwa ya magari ya Marekani ya GM.

Hatua hiyo imekuja baada ya makisio ya mauzo ya bidhaa za Opel kwa mwaka ujao kukadiriwa kushuka nchini Uingereza kutokana na hatua maarufu ya ‘Brexit’.

Dalili za kuporomoka kwa uchumi wa Uingereza na biashara kwenye nchi hiyo zimeanza kuonekana huku thamani ya Paund ikidorora dhidi ya Dola na Euro tangu Uingereza itangaze uamuzi huo Juni 23 hivyo kupelekea ongezeko la gharama za usafirishaji kwa makampuni ya nje ya Uingereza.

Uingereza imekuwa soko kubwa la gari zinazotengenezwa na Opel aina ya Insignia na Corsa.

Gari za Opel huuzwa nchini Uingereza kwa kutumia jina la kibiashara la Vauxhall.

Hata hivyo msemaji huyo wa Opel hakufafanua ni kwa kiasi gani muda huo utapunguzwa.

Hatua ya Opel haionekani kuwa mpya ingawa inaonekana kuongeza athari kwa wafanyakazi wengi zaidi huku kampuni nyingine ya magari kutoka Ujerumani ya Volkswagen ikiwa imeshaanzisha utaratibu huo kwenye karakana zake kadhaa lakini ikitumia sababu tofauti ya kufanya hivyo.

 

LEAVE A REPLY