Breaking New: Roma na wenzake wapatikana wakiwa hai

0
369

Mwanamuziki wa hip hop, Roma na wenzake waliotekwa wakiwa studio za Tongwe zilizopo Masaki jijini Dar es Salaam wamepatikana wakiwa hai.

Taarifa zilizoenea katika mitandao ya kijamii zinasema kuwa wanamuziki hao kwasasa wapo kituo cha Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam wakitoa maelezo kuhusu sakata hilo.

Roma na wenzake walitekwa siku ya Jumatano katika Studio za Tongwe na watu wasiojulikana bila kujua sababu.

Habari ya kupatikana wakina Roma imethibitishwa na Mkurugenzi wa Tongwe Records J. Murder.

Bado hakuna maelezo ya kutosha kuhusiana na wapi walipokuwa na nani waliokuwa wamewashikilia.

Kwa sasa wanadaiwa kuwepo kituoni hapo kwa taratibu za kipolisi kwa kuwa jalada la kupotea kwao lilifunguliwa hapo.

Kupatikana kwao kumefuatia wito mkubwa uliokuwa ukipaishwa na wasanii wenzake na mashabiki kuhusu kuachiliwa huru, ndani na nje ya mitandao ya kijamii.

Kwa habari zaidi endelea kukaa na tovuti hii kujua zaidi.

LEAVE A REPLY