BREAKING NEWS: Pogba ‘SHETANI’ mpya Old Trafford?

0
112
during the Serie A match between Juventus FC and AC Chievo Verona at Juventus Arena on January 25, 2015 in Turin, Italy.

Gazeti la SUN la Uingereza limeripoti kuwa Juventus na Manchester United zimeafikiana bei ya mchezaji wa kimataifa wa Ufaransa, Paul Pogba.

Taarifa hiyo ya faraja kwa Mashetani Wekundu imechapishwa toleo la leo la gazeti hilo baada ya waandishi wake kufanya mahojiano na mmoja wa viongozi wa juu wa klabu ya Juventus aliyewathibitishia kuwa ‘DEAL DONE’.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya Juventus kulegeza uzi na kukubali kuchangia £4m kwenye malipo ya wakala wa Pogba, Mino Raiola.

Manchester United wameamua kuharakisha makubaliano hayo na kukubali kulipa sehemu kubwa ya ada ya wakala wa Pogba baada ya kuzuka kwa tetesi kuwa Real Madrid wameanza upya jitihada za kumtwaa staa huyo wa Ufaransa.

Makubaliano baina ya pande tatu zilizokuwa zikivutana yalifikia tamati baada ya Raiola kufanya kikao na mkurugenzi wa ufundi wa Juventus, Beppe Marotta juzi.

Bei kamili ya mauzo ya Paul Pogba inatarajiwa kufikia £112m na kumfanya kuwa mchezaji ghali zaidi duniani.

Inaaminika kuwa Juventus imekubali kumuuza Pogba ili kurudisha pesa ‘ndefu’ £79m waliyoitumia kumnunua mshambuliaji, Gonzalo Higuain kutoka Napoli.

LEAVE A REPLY