Breaking News: Wanajeshi 7 wa UN miongoni mwa watu 13 waliouawa Mogadishu

0
199

Kundi la Al-Shabaab limetangaza kuhusika na mauaji ya watu 13 yaliyotokea mapema leo kwenye mji mkuu wa Somalia, Mogadishu.

Mauaji hayo yametokea baada ya magari mawili yaliyokuwa ya mabomu yalipolipuka wakati yakiendeshwa kuelekea kwenye kambi ya vikosi vya jeshi la Afrika.

‘Wapiganaji wetu waliilenga Halane ambayo ni ngome ya majeshi ya kigeni ambayo yameivamia nchi yetu ya kiislam. Tumewaua wengi wao’. Amesema msemaji wa kundi hilo Abdulaziz Abu Muscab

Mlipuko wa kwanza umetokea karibu na geti la kuingilia kwenye kambi ya vikosi vya jeshi la Afrika na mlipuko wa pili umetokea kwenye eneo la ukaguzi ambalo liko chini ya majeshi ya serikali ya Somalia.

Kapteni wa polisi wa kicks cha Somalia, Mohamed Hussei amethibitisha kuwa wanajeshi 7 wa Umoja wa Mataifa wamefariki dunia kufuatia shambulizi hilo la bomu.

LEAVE A REPLY