Branislav Ivanovic ajiunga Zenit St Petersburg

0
87

Hatimaye mlinzi wa pembeni wa miamba ya soka ya Uingereza, Chelsea, Branislav Ivanovic amejiunga na miamba ya Urusi Zenit St Petersburg.

Uhamisho huo uliokamilishwa mapema leo haujaweka wazi kiasi cha ada iliyokubaliwa baina ya vilabu hivyo, Ivanovic amesaini mkataba wa miaka miwili na nusu.

Ivanovic aliyejiunga na Chelsea mwaka 2008 akitokea Lokomotiv Moscow na ameichezea timu hiyo jumla ya michezo 377.

Akiwa na Chelsea Ivanovic amefanikiwa kutwaa mataji makubwa ya nchini Uingereza na Ulaya ikiwemo ubingwa wa klabu bingwa Ulaya, ligi kuu ya Uingereza (2), kombe la FA (3) na kombe la ligi (1) huku akiwa ndiye mfungaji wa bao la ushindi kwenye fainali ya kombe la Europa.

Pamoja na mafanikio hayo, Ivanovic hakuwa na msimu mzuri mwaka huu na amefanikiwa kucheza mara sita tu kwenye michezo ya ligi kuu ya Uingereza.

Nahodha wa Chelsea, John Terry amekuwa mchezaji wa kwanza kuonyesha heshima yake kwa mchezaji huyo na kuandika kwenye mtandao wa Instagram:

‘Legend’ “Unbelievable defender for us over the years and a great and big character and presence in the dressing room’.

LEAVE A REPLY