Botswana wamtaka Kabila kuachia madaraka

0
78

Serikali ya Botswana imesema kuwa Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo ndiyo chanzo cha ukiukwaji wa haki za binadamu na kuzorota kwa hali ya usalama.

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa imemkosoa Kabila kwa kuendelea kubaki madarakani huku ikitoa wito kwa Jumuiya ya Kimataifa kuongeza shinikizo dhidi ya kiongozi huyo ambaye alipaswa kuondoka madarakani Desemba 2016.

Mbali ya Botswana kumlaumu Kabila, pia imewakosoa viongozi wengine wa Afrika ambao wameamua kubadili Katiba za nchi zao ili waendelee kubaki madarakani.

Viongozi hawa sasa wameamua kutumia njia kama vile kuchelewesha kufanya chaguzi au mabadiliko ya Katiba za Taifa kwa lengo la kuendelea kubaki madarakani.

Ni wazi kwamba viongozi kama hawa wanaongozwa na maslahi yao binafsi badala ya kujali maslahi ya taifa. Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo ni mfano kuntu. Tunaendelea kushuhudia kuzorota kwa haki za binadamu katika nchi hiyo na sababu kubwa ni kiongozi wake mkuu kuendelea kuchelewesha uchaguzi huku akiwa amepoteza udhibiti wa vyombo vya usalama.ö

Botswana ina uthabiti wa kimaadili wa kuzinyoshea kidole nchi nyingine kwa sababu Rais wake Ian Khama aliyeingia madarakani mwaka 2008 alitangaza Novemba mwaka jana kuwa atangaza Aprili mwaka huu na kumwachia ofisi makamu wake Mokgweetsi Masisi kuongoza hadi uchaguzi mkuu mwaka 2019.

LEAVE A REPLY