BOT yasema uchumi wa nchi bado upo imara

0
158

Gavana wa benki kuu ya Tanzania BOT, Prof Benno Ndulu amesema hali ya uchumi nchini imeendelea kuridhisha japo katika robo ya kwanza ya mwaka huu kasi ya ukuaji wa pato la taifa imefikia asilimia 5.5 ikilinganishwa na ongezeko la asilimia 5.7 ya kipindi kama hicho mwaka 2015.

Ametoa kauli hiyo mbele ya waandishi wa habari katika moja ya kumbi za BOT alipokuwa na mada inayohusu kushuka kwa uchumi na aliweza kutoa ufafanuzi.

Gavana amesema “Hali ya ukuaji ya uchumi Tanzania bado ni nzuri na Tanzania bado ni katika nchi kumi bora kwa matarajio pia,’.

Pia amesema viashiria vitakavyoimarisha uchumi kwa mwaka 2016 ni pamoja na miradi mikubwa inayotekelezwa hapa nchini na kuongezeka kwa malighafi.

Aliongeza kwa kufafanua kwamba “Ujenzi wa reli ya kati ambao utaanza muda sio mrefu, wenyewe kwa mwaka huu tunategemea uanze kwa kilometa mia 200 za kwanza na itatumia pesa kiasi kingi, na itatumia simenti,itatumia nguvu kazi katika kuhakikisha mradi huu unatekelezwa na chanzo kimoja cha ukuaji ni uwekezaji,”.

Kuhusu fedha kupotea mikononi mwa watu gavana huyo amesema, “kuzungumzia suala la mabadiliko la fedha nani mwenye fadha mfukoni, fedha nyingi zilizokuwa zikitumika vibaya zimerudi zinasaidia umma moja kwa moja na sio maana yake unawagawia hapana, kama ni elimu, kujenga madarasa, madawati na vitu hivi vyote bado kuna watu watapata shughuli ya kufanya.”

LEAVE A REPLY