BOOM milioni 90: Ni followers wa Katy Perry on TWITTER!!

0
182

Staa wa muziki kutoka Marekani, Kate Perry amekuwa msanii na mtu wa kwanza duniani kuwa na wafuasi wengi zaidi kwenye mtandao wa Twitter.

Perry amefikisha wafuasi milioni 90 kwenye mtandao huo hiyo ikiwa ni historia pia kwa mtandao huo tangu uanzishwe miaka 10 iliyopita.

‘Hivi karibuni alikaririwa akisema kuwa: Unapokuwa na mashabiki elfu 90 kila mahali wakiwa nawe, kila neno unalolisema wanalisikiliza, kosa moja tu litakugharimu’.

‘Pindi unapokuwa na jambo kubwa la kupoteza unakuwa mwangalifu zaidi kwasababu kadri unavyokuwa mkubwa ndivyo inavyokuwa viguu kuanguka. Nadhani dunia imefikia mahala inakuamulia nini uzungumze na nini usizungumze. Na sio mimi tu, ni kila mmoja’

 Single ya staa huyo, ‘Rise’ imekuwa ikitumika kama soundtrack kwa wachezaji wa Marekani kwenye mashindano ya Olimpiki yaliyomalizika juzi.

LEAVE A REPLY