Boko Haram washambulia msafara wa UN

0
78
Wapiganaji wanaodhaniwa kutoka katika kundi la Boko Haram wameuvamia msafara wa Umoja wa Mataifa uliokuwa umebeba misaada ya kibinadamu huku ukisindikizwa na wanajeshi wa umoja huo.
Shambulizi hilo limetokea kaskazini-mashariki mwa nchi hiyo na kusababisha wanajeshi wawili na raia watatu akiwemo afisa wa UN kujeruhiwa.
Hali hiyo imepelekea Umoja wa Mataifa kusitisha utoaji wa misaadakwenye jimbo la Borno ambako zaidi ya watu milioni mbili wamekosa makazi kutokana na wapiganaji hao.
Kwenye taarifa yake ya hivi karibuni Umoja wa Mataifa umelaani vikai matendo ya kinyama na yasiyotumia akili yanayofanywa na kundi la Boko Haram ambayo yamesababisha maelfu ya watoto wadogo kukumba na utapiamlo mkali kutokana na ukosefu wa chakula.
Mapema mwezi huu, Umoja wa Mataifa ulionya kuwa maelfu ya watoto watafariki iwapo hawatopatiwa msaada wa haraka wa matibabu.
Kwa miaka 7 ya mapigano na serikali ya Nigeria, kundi la Boko Haram limesababisha mauaji ya watu 20,000 wengi wao wakitokea kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.
Karibu watoto 250,000 wameathiriwa na utampiamlo mkali kwenye nchi hiyo na takwimu za Umoja wa Mataifa zinaonyesha kuwa mtoto mmoja katika kila watoto watano yuko katika hatari ya kufariki dunia endapo hatopata msaada wa matibabu na chakula mapema.

LEAVE A REPLY