Bocco achaguliwa kuwa mchezaji bora mwezi Januari

0
165

Mshambuliaji wa Simba, John Bocco amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa mwezi Januari wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL)Tanzania Bara.

 Bocco ambaye pia ni nahodha wa Simba alitwaa tuzo hiyo baada ya kuwashinda wenzake wawili, mshambuliaji Emmanuel Okwi wa Simba na Awesu Awesu wa Mwadui.

 Kiwango cha mshambuliaji huyo aliyecheza dakika zote 270 za michezo mitatu ya Simba mwezi huo kilikuwa juu karibu kila mchezo.

Kutokana na ushindi huo, Bocco atazawadiwa tuzo, kisimbuzi cha Azam na fedha taslimu sh. milioni moja kutoka kwa Mdhamini Mkuu wa Ligi, Kampuni ya Vodacom Tanzania.

 Wachezaji wengine ambao tayari wameshinda Tuzo ya Mchezaji Bora wa mwezi wa VPL msimu huu na miezi yao katika mabano ni Okwi (Agosti), beki wa Singida United, Shafiq Batambuze (Septemba) na mshambuliaji wa Yanga, Obrey Chirwa (Oktoba).

LEAVE A REPLY