Bob Junior kurudi kwenye game

0
333

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Bob Junior amefunguka na kusema kuwa ukimya wake ulisababishwa baada ya kurejea shule.

Akizungumzia kupotea kwake kwenye game ya muziki, Bob Junior amesema kuwa alikuwa kimya kwenye muziki kwa sababu aliamua kurudi shule kujiendeleza kielimu.

” Ukimya wangu ulitokana na Mosomo, wazazi wangu hawakutaka nifanye Muziki bila Elimu, Wakati nasoma nimeandika zaidi ya nyimbo 60. Na elimu yangu nimesomea Finland Masuala ya Telecommunication.“

Kuhusu Mahusiano yake na Diamond Platnumz, Bob Junior ameeleza kuwa wana mahusiano mazuri na wameshafanya ‘Project’ ya pamoja ambayo itatoka mwezi wa 12 mwaka huu.

” Mimi na Diamond Platnumz tulisaidiana Sana Ndio Maana wote tupo hapa na tunajulikana, na hakuna beef lolote kati yetu, tunaelewana sana na kuthibitisha hilo kuna ngoma ambayo tumefanya pamoja ambayo tutaitoa mwezi wa 12 mwaka huu.” Ameeleza Bob Junior.

LEAVE A REPLY