Bob Junior azidi kumchana Tunda Man

0
273

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Bob Junior amesema kuwa Tunda Man amemzidi umri tu lakini kwenye muziki yeye ni mkubwa zaidi yake.

Bob Junior amesema kuwa muziki ameanza muda mrefu lakini wazazi walikuwa wakimzuia na kusisitiza asome kwanza kwa kuwa alikuwa bado mdogo.

Pia amesema kuwa “Tunda ni kaka yangu na nina mheshimu kwakuwa kanizidi umri na baadhi ya vitu lakini kwenye kazi tuheshimiane mie sio mtoto kama anavyosema mbona nmemfanyia baadhi ya nyimbo zake tena bure wakati anaanza, sasa nani mdogo hapo kati yetu”,.

Hayo yamejiri baadaya msanii Tunda Man kutoa video tatu za nyimbo zake mpya suala ambalo lilimuibua Bob Junior na kutoa ushauri kwa msanii huyo kuwa alitakiwa kutoa kwa awamu ili awape muda mashabiki wake.

LEAVE A REPLY