Blue adai hana bifu na Diamond Platnumz

0
260

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Mr Blue amedai kuwa hana bifu na msanii mwenzake Diamond Platnumz kama inavyosambazwa katika kitandao ya kijamii.

Blue amefunguka hayo baada ya habari kusambaa kuwa wawili hao wanatofauti baada ya kugombania jina la Simba ambapo hadi sasa Diamond analitumia kama A.K.A yake.

Mr Blue amesema kuwa watu ndio wanataka kuwaingiza kwenye matatizo, ila yeye ndio ameanza kumsupport Diamond tangu chini kabisa akiwa hajulikani na mtu yoyote hata waandishi wa habari.

Blue amesema kuwa kama ningekuwa na tofauti ningemzuia tokea awali hata nyinyi msingepata ajira, kama ningemzuia kule mwanzoni nisinge msupport.

Pia Blue amesema kuwa Diamond ni kama mdogo wake wakati anatoka hakuwahi kuwa na bifu naye wala hakuwahi kukaa chini kumwambia anatofauti naye.

LEAVE A REPLY