Binti wa Obama aanza kazi mgahawani

0
468
Sasha Obama watches a folk dance by performers during her visit at the City Wall, in Xi'an, Shaanxi province, March 24, 2014. REUTERS/Petar Kujundzic (CHINA - Tags: POLITICS TRAVEL) - RTR3IBRY

Binti mdogo wa rais wa Marekani, Sasha Obama ameamua kuwafundisha watoto wanaotoka kwenye familia za watu wa daraja la juu kuwa ‘mamlaka au uwezo wa wazazi wao sio kigezo cha kuwafanya wao kudharau au kuchagua kazi’ kwa kukubali kufanya kazi ya uhudumu kwenye mgahawa wa vyakula vya baharini.

Binti huyo mwenye miaka 15 amekubali kufanya kazi katika mgahawa wa Martha’s Vineyard uliopo kwenye jimbo la Massachusetts katika kipindi cha kiangazi nchini Marekani.

Hata hivyo inadaiwa kuwa binti huyo ambaye kwenye mgahawa huo anatumia jina lake kamili la Natasha amekuwa akisindikizwa na maafisa sita wa idara ya usalama wa taifa ya nchi hiyo.

Jimbo la Massachusetts limekuwa maarufu kw afamilia ya Obama kulitumia kwenye likizo za kipindi cha kiangazi.

Mmoja wa wafanyakazi wa mgahawa huo ameeleza kuwa mwanzoni hawakuwa wakifahamu Natasha ni nani na walikuwa wakishangaa kuona watu sita wakimsaidia kwenye mambo kadhaa lakini baada ya kufuatilia waliweza kufahamu hadhi ya binti huyo.

Ikulu ya Marekani bado haijaeleza chochote kuhusu habari hiyo ingawa mama wa binti huyo na mke wa rais Obama, michelle Obama aliwahi kunukuliwa akisema kuwa yeye na mumewe wanafanya jitihada kubwa ya kuwafanya watoto wao wajifunze kuishi maisha ya kawaida.

Sasha ameingia kwenye orodha ya watoto kadhaa wa matajiri na watu maarufu kufanya kazi za kawaida ambapo kwenye orodha hiyo yupo pia dada yake Malia ambaye aliwahi kufanya kazi kwenye kampuni ya kutengeza filamu, pia yupo mtoto wa staa wa soka David Beckham, Brooklyn Beckham ambaye aliwahi kufanya kazi kwenye studio za kutengenezea filamu za mkongwe, Guy Ritchie jijini London.

LEAVE A REPLY