Bilnass athibitisha Nandy mkewe kisheria

0
64

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Bilnass amefunguka na kuthibitisha kuwa kuwa yeye na mpeniz wake Nandy ni mtu na mkewe baada ya kuishi naye kwa muda mrefu.

BillNass amesema kuwa muda mwingi wanakuwa wote japo kila mtu anaishi kwake. “Kwenye jicho la kisheria huyu tayari ni mke wangu, kwa sababu mara nyingi tupo pamoja japo huyu ana kwake na mimi nina kwangu lakini muda mwingi tunakuwa Pamoja.

Mapema mwezi wa nne mwaka huu wawili hao waliweka hadharani mahusiano yako kwa kuveshana pete ya uchumba.

Pia Billnass aanika wazi kwamba Nandy anaingiza pesa nyingi zaidi yake. Kwenye mahojiano na kipindi cha Leo Tena Clouds FM, Nenga amesema Nandy anapata shoo nyingi na pia ana miradi mingi zaidi yake.

Billnass amesema kuwa ni Nandy lakini akaenda mbali na kufafanua kuwa yeye ndio mwenye fedha nyingi zaidi ya Nandy kutokana na matumizi ya mchumba wake huyo.

Nandy anaingiza pesa zaidi yangu, anapata shoo nyingi na ana miradi mingi. Lakini mwisho wa siku tukiwa tunafanya tathimini za nani ana pesa nyingi kwenye akaunti, mimi ndio nakuwa juu,” amesema billnass na kuongeza.

Hiyo inatokana na kuwa Nandy ana matumizi mengi kuliko mimi, kwa hiyo huingiza pesa nyingi lakini pia hutumia pesa nyingi zaidi.” alimaliza Billnass ambaye safari hii ameshirikishwa na Nandy kwenye ‘Do Me’ wimbo wao mpya unaofanya vizuri kwa sasa.

LEAVE A REPLY