Billnass akanusha kukataliwa ukweli

0
120

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Billnass amefunguka na kukanusha kuwa wazazi wa Nandy hawamtambui licha ya kumvalisha pete ya uchumba.

Kauli ya mwanamuziki huyo imekuja baada ya Billnass kumvisha pete ya uchumba Nandy kwenye kipindi cha Homa kinachorushwa na kituo cha Televison cha TV E na baadhi ya watu kuanza kusema kuwa Billnass ajakubaliwa na wazazi wa Nandy.

Billnass amesema kuwa haoni tatizo yeye kumfanyia surprise mpenzi wake kwa sababu hicho ndicho kitu anachokipenda.

“Unajua ukikaa na kuanza kusikiliza maneno ya mtandaoni, utaumiza akili yako bure, kwa sababu asilimia kubwa ya watu wanaoongea hivyo, hawajitambui vizuri.

Pia Billnass amesema kuwa “Kuhusu kukataliwa ukweni, sidhani kama ni kweli, lakini pia wakwe zangu mimi ni watu wa dini sana, hivyo nisingependa kuwaongelea sana kwenye media yoyote ile kwa sababu ninachokijua mimi ni kwamba, wananipenda kama mtoto wao na wamenikubali.”

Billnass na Nandy wametoka mbali, waliwahi kuwa wapenzi wakaachana na sasa wamerudiana kwa kasi na jamaa kaona amvishe pete kabisa.

LEAVE A REPLY