Billnass akanusha bifu na Dogo Janja

0
126

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Billnass amefunguka na kusema kuwa hana bifu na mwanamuziki wake Dogo Janja licha kutupiana maneno katika mitandao ya kijamii.

Kauli ya mwanamuziki huyo inakuja baada ya kuambiwa na mashabiki wao kuwa wana bifu kutokana na kutupiana maneno ya kejeli katika mtandao wa Instagram siku chake zilizopita.

Wanamuziki hao walitupiana maneno ya kejeli ambayo yalizua gumzo kwamba wawili hao wana bifu kutokana na meneno hayo waliyokuwa wanarushiana.

Awali Dogo Janja aliandika maneno kwenye ukurasa wa Billnass ambayo yalisomeka hivi; ‘Wewe ndiyo maana uliachwa na dada una mdomo sana, hamna mwanamke anaweza kukaa na mwanaume anachamba kuliko mwanamke’,.

Baada ya muda Billnass naye alijibu kwa kuandika; ‘bora kuachwa kuliko kuolewa na mwanamke ili ucheze na mwanaye yeye akienda outings’.

Billnass amesema kuwa hana bifu na Dogo Janja, hayo maneno waliyokuwa wanaandikiana yalikuwa ni utani tu kwani wameshazoea kutaniana.

LEAVE A REPLY