Billnass afuta picha zote kwenye Instagram yake

0
59

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Billnass ameaondoa picha na video zote kwenye ukurasa wake wa Instagram, hatua iliyohisiwa kuwa ni maandalizi ya kuachia kazi mpya hivi karbuni.

Billnass amefuta picha hizo lakini bila kusema sababu yoyote ila wadadisi wa mambo wanasema kuwa uhenda anataka kuachia nyimbo mpya.

Hatua hii ya Billnass imevuta hisia za baadhi ya mashabiki ikihisiwa kuwa huwenda akaachia wimbo mpya baada ya kufanya vizuri na wimbo ‘Do Me’ alioshirikishwa na Nandy.

Uamuzi wa Bill Nass hakujali hata picha alizopiga na Mpenzi wake, Nandy huku upande mwingine ikihisiwa kuwa pengine kuna kingine kisichohusiana na ujio wa kazi kutoka kwake.

LEAVE A REPLY