Bibi yake Obama kuendelea kupewa ulinzi nchini Kenya

0
200

Bibi wa aliyekuwa rais wa Marekani Barack Obama, Sarah Obama ataendelea kupewa ulinzi wa serikali licha ya kumalizika kwa utawala wa mjuu wake nchini Marekani.

Nyumbani kwa Sarah Obama katika kijiji cha Kogelo kaunti ya Siaya mashariki mwa Kenya, kuliwekwa ua na baadaye chini ya ulinzi wa polisi wakati mjukuu wake alichaguliwa kuwa rais wa 44 wa Marekani.

Wageni wataoingia nyumbani kwa Sarah watahojiwa katika kituo hicho cha polisi kilicho nje ya boma lake.

Mkuu wa polisi eneo hilo, Joseph Sawe aliliambia gazeti la Standard kuwa watamtembelea Bi Sarah Obama kujua vile anaendelea.

Kijiji cha Kogelo kinaendelea kuwavutia watalii ambao wangependa kuona alikotoka babake Obama, ambaye amemzungumzia katika kitabu chake Dreams From My Father.

LEAVE A REPLY