Biashara ya ngozi ya Punda ‘marufuku’ Burkina Faso

0
331

Serikali ya Burkina Faso imepiga marufuku biashara ya kimataifa ya ngozi ya Punda.

Serikali hiyo imekomesha biashara hiyo baada ya kushamiri kwa kasi baina ya wafanyabiashara wa nchi hiyo na wenzao wa China.

Biashara hiyo ya ngozi za Punda imeshika kasi nchini humo kuanzia mwaka 2015 ambapo zaidi ya ngozi 65,000 zimesafirishwa kwenda China kwenye kipindi cha miezi 6 iliyopita.

Mamlaka za Burkina Faso zimeonya kuwa kwenye robo ya mwanzo ya mwaka 2015 ngozi zilizouzwa nje zilikuwa 1,000 lakini kwenye robo ya mwisho wa mwaka huo ngozi zaidi ya 18,000 zilikuwa zimesafirishwa.

Marufuku hiyo imeanza kufanya kazi kuanzia Jumanne inajumuisha pia marufuku ya uuzwaji nje ya nchi wa ngozi za ngamia na farasi.

Nchini Burkina Faso, Punda ni mashuhuri sana kwa biashara ya usafirishaji mizigo huku kwenye baadhi ya jamii akitumiwa kama chakula.

Kushamiri kwa biashara hiyo ya usafirishaji wa ngozi za Punda umesababisha bidhaa hizo kupanda bei hadi kufikia $51.

LEAVE A REPLY