Beyonce kutumbuiza harusi ya Bale

0
120

Mwanamuziki wa Marekani, Beyonce anatarajia kutumbuiza kwenye harusi ya mchezaji wa Real Madrid, Gareth Bale kwa kiasi cha shilingi bilioni 4.4.

Bale anategemea kumwoa mpenzi wake wa siku nyingi, Emma Rhys-Jones, ambapo anataka mwanamuziki huyo wa kundi lililokuwa linajulikana kama Destiny’s Child awaburudishe waalikwa.

Ndoa hiyo iliyotakiwa kufanyika nchini Italia mapema, ilichelewa kutokana na baba wa Rhys-Jones kufungwa kutokana na utapeli nchini Marekani.

Wawili hao wamefahamiana tangu utotoni na wanaishi jijini Madrid na watoto wao wa kike wawili. Baada ya sherehe hiyo huko Italia, wamepanga kufanya sherehe nyingine huko Wales.

Bale ana mkataba na Real Madrid ambapo analipwa Sh. milioni 894 kwa wiki (Paundi 300,000) na anasemekana anaweza kuhama kwenda Manchester United ya Uingereza. Beyonce, aliyeoana na nyota wa muziki wa hip-hop, Jay-Z mwaka 2008, ameuza rekodi zipatazo milioni 100 akiwa msanii anayejitegemea.

LEAVE A REPLY