Beyonce ‘kitumbo’ kuperform Grammy

0
317

Staa wa Pop wa Marekani, Beyonce amekubali kufanya performance kwenye utoaji wa tuzo za Grammy licha ya kuwa mjazito wa watoto mapacha.

Baba mzazi wa staa huyo, Mathew Knowles ndiye aliyetoa taarifa hiyo wakati alipokuwa akihojiwa na kipindi cha televisheni cha US TV, ambapo alidai staa huyo anajisikia uchovu sana kwa sasa kwasababu amekuwa akifanya mazoezi kwaajili ya onyesho hilo.

Baba huyo pia amedai kustushwa na habari kuwa mtoto wake ni mjazito kwakuwa hakuwa na taarifa na alikuja kuzithibitisha habari hizo alipoziona kwenye ukurasa wa mwanae wa Instagram.

Beyonce amechaguliwa kuwania vipengele tisa vya tuzo za Grammy mwaka huu.

Mastaa wengine watakaoperform kwenye tuzo hizo ni pamoja na Adele, Bruno Mars, the Weeknd, Daft Punk na Alicia Keys zitakazofanyika kwenye jiji la Los Angeles Jumapili ya Februari 12.

LEAVE A REPLY