Beyonce ajifungua watoto mapacha

0
389

Mwanamuziki nyota wa Marekani,  Beyonce amejifunga salama watoto mapacha ambao amezaa na mumewe  J-Z.

Kulikuwa na siku za mijadala katika mitandao ya kijamii kuhusu kujfungua kwa mwanamuziki nguli mwenye miaka 35 katika kituo kimoja cha afya huko Los Angeles nchini marekani.

 Mdogo wa mwanamziki huyo, Solange Knowles alionekana akirandaranda kwenye kituo hicho cha afya, ndipo mapaparazi walipojisogeza ili kufahamu undani wa jambo hili.

Mwanzoni mwa mwaka huu mwanadada huyu alipiga picha mbele ya ua kubwa huku kashikilia tumbo lake na kupost kwenye ukurasa wake wa instagram kwamba wamebarikiwa kwa kutarajia kuleta zawadi nyingine.

Supastar wa miondoko ya Hip Hop Jay Z, mwenye miaka 47 Jumanne iliyopita alionekana akiondoka kwenye kasri lao lililopo Beverly Hills na kuelekea kwenye kituo hicho cha afya na mara ulinzi katika kituo hicho uliimarishwa.

LEAVE A REPLY