BET AWARDS: Drake kwenye vipengele 14

0
83

Mwanamuziki supastaa, Drake amezitawala tena tuzo za mwaka 2016 za BET hip-hop awards kwa mwaka wa 3 mfululizo.

Rapa huyo kutoka Canada anawania tuzo 14 kwenye tuzo hizo.

Amechaguliwa kuwania tuzo za Albamu bora ya mwaka na

Mtumbuizaji bora jukwaani miongoni mwa tuzo anazowania.

Tuzo za mwaka huu za BET zinatarajia kutolewa katikati ya mwezi Oktoba mwaka huu lakini zitaonyeshwa kwa mashabiki katikati ya mwezi ujao.

Ngoma ya Drake One Dance bado kidogo imuwezeshe kufikia rekodi ya ngoma ya mkongwe Bryan Adam, Everything I Do ya kukaa kwenye kilele cha chati za Official Singles Chart kwa wiki 16.

One Dance ilikaa kileleni mwa Official Singles Chart kwa wiki 15 mwanzoni mwa mwaka huu.

Albamu yake ya mwisho pia imefanikiwa kuka kileleni kwa wiki 12 kwenye chati za albamu 200 bora za Billboard.

Msanii Future ambaye aliachia albamu ya pamoja na Drake ndiye anayeshika nafasi ya pili kwa kutokea kwenye vipengele 10.

 

LEAVE A REPLY