Beni: Zaidi ya watu 30 wauawa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo

0
369

Zaidi ya raia 30 wameuawa nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo katika shambulizi mashariki mwa taifa hilo.
Msemaji wa jeshi nchini humo, Mark Azuray ameambia shirika la habari la AFP kuwa mauaji hayo yalitokea katika mji wa Beni nyakati za usiku.
Wanajeshi wanashuku kuwa kundi la wanamgambo la ADF lilitekeleza mauaji hayo.
ADF ni kundi la kujihami lililo na asili yake nchini Uganda, na linaendeleza shughuli zake karibu na mpaka.

LEAVE A REPLY