Ben Pol afunguka ndoa na mpenzi wake Annerlisa

0
123

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Benpol amefunga ndoa ya kanisani na mpenzi wake wa muda mrefu, Annerlisa, ambaye ni raia wa Kenya.

Picha za ndoa hiyo zimeanza kusambaa mitandaoni hivi karibuni lakini wanandoa hao hawajaposti chochote kuhusu tukio hilo adhimu lakini pia hawajazungumza popote kuhusu ndoa yao hiyo.

Ben Pol na Anerlisa walifunga ndoa yao kwa siri kubwa, jijini Dar es Salaam nchini Tanzania mwezi Juni mwaka huu ambapo kilikuwa kipindi cha Covid 19, kwani hata picha za Kanisani zinaonyesha hakuna watu.

Ben Pol aliwahi kuthibitisha kuwa kila kitu kilikuwa tayari kwa ajili ya kufunga ndoa na mpenzi wake huyo ambaye waliingia kwenye mahusiano mwaka 2018 na kuutangazia umma mwaka 2019, kwani taratibu zote za kimila zilishafanyika.

“Mimi na Anerlisa tuna mipango mingi mbeleni. Nishamlipia hadi mahari, lakini sidhani kama nitakuwa sahihi nikitaja ni mahari kiasi gani nimelipa kwao. Tumefanya taratibu zote za kimila. Nyumbani kwao tumeshakamilisha kila kitu. Kilichobaki ni zile taratibu za Kizungu tu,” alisema Ben Pol.

LEAVE A REPLY