Ben Pol afunguka kuhusu upendo wa mpenzi wake

0
69

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Ben Pol amefunguka na kusema moja ya sababu inayofanya watu kuzungumzia sana penzi lake ni kutokana na kuwa na mwanamke mzuri ambaye amebadilisha maisha yake kwa sasa.

Ben Pol amesema kuzungumziwa kwake inatokana na mpenzi wake kuwa mzuri hivyo hawezi kuacha kumzungumzia mpenzi wake huyo kutoka nchini Kenya.

“Kwanza nadhani watu hawajanizoea kwa kuweka mahusiano yangu hadharani, kwahiyo imeleta mitazamo tofauti kwa mashabiki wake.

Pia amesema kuwa “Mpenzi wangu anaongelewa kiupande wake kwa kule kwao na hata huku kuna Watanzania ambao walikuwa wanamfuatilia kwa muda mrefu, halafu ni mtu maarufu  na kitu kingine ni mzuri”.

Pia mwisho amesema kuwa  “Ameniweka karibu na Mungu zaidi, ameniongezea utu na ubinadamu wa kawaida, ananisaidia katika mawazo ya kazi, ana sikio zuri la muziki, jicho la fashion, na tunasaidiana kwenye kazi zetu”.

LEAVE A REPLY