Ben Pol afunguka alipokutana Anerlisa

0
113

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Ben Pol amefunguka na kueleza kila kitu kuhusu mpenzi wake Anerlisa raia wa Kenya ambaye wapo kwenye mahaba mazito.

Ben Pol amezungumza kuanzia kukutana naye hadi kumtolea mahari mpenzi wake raia wa Kenya ambaye kwasasa wanaishi wote nchini Kenya.

Ben Pol amesema kuwa alikutana na Arnelisa mwaka 2018 mwanzoni wakati alipokwenda Kenya kikazi wakakutana kwenye Press Conference iliyoandaliwa na rafiki yake nchini Kenya.

Ben Pol ameendelea kusema kuwa wakati huo hakuwa anamfahamu wala kujua anafanya nini lakini yeye alikuwa anamfahamu kwasababu watu wa Kenya wanasikiliza sana muziki wa Kenya.

Pia ameongeza kwa kusema kuwa akaongea na tukabadilishana namba na mengine yakafuata. Mwanzo sikuwa na nia ya kimahusiano kwake, nilikuwa navutiwa na vibe lake kwenye stories” amesema Ben Pol na kuongeza;

“Mimi na Anerlisa tuna mipango mingi mbeleni, nishamlipia hadi Mahari lakini sidhani kama nitakuwa sahihi nikitaja ni mahari kiasi gani nimelipa kwao! Tumefanya taratiu zote za kimila nyumbani kwao tumeshakamilisha kila kitu kilichobaki ni zile taratibu za kizungu tu.” alimaliza Ben Pol.

LEAVE A REPLY